PlaneteAfrique
Déconnexion
WS-Apps, le système de gestion de contenus adaptatif développé depuis 15 ans, conçu pour sa puissance, son efficacité et sa simplicité. Trois applications, une présence web maîtrisée :
WS-MySite! Votre présence web immédiate et professionnelle. Découvrir ce pack
WS-Webzine Pour agences de presse et éditeurs. Découvrir ce pack
WS-Ecommerce Vendez en ligne et encaissez par Mobile Money et carte bancaire. Découvrir ce pack

Watanzania waombwa kutunza amani

Watanzania waombwa kutunza amani


Viongozi na wafanyakazi wa mashirika mbalimbali walioshiriki kuwarejesha kwao wakimbizi wa Burundi waliokuwa wakihifadhiwa katika kambi ya Mtabila wilayani Kasulu wamewaomba watanzania  kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuvuruga amani hapa nchini.



Wakizungumza baada ya kukamilisha kazi ya kuwarejesha kwao wakimbizi wa Burundi wamesema kuwa maisha ya ukimbizini waliyoyashuhudia ni ya shida na ghadhabu nyingi, hivyo watanzania wanapaswa kuhakikisha kuwa amani iliyopo  nchini haipotei.



Baadhi ya viongozi wa serikali na wafanyakazi wa  mashirika ya kitaifa na kimataifa wameshuhudia familia ya mwisho ya mkimbizi wa Burundi akipanda basi kurejea kwao.



Hata hivyo pamoja na mafanikio ya kukamilisha kazi ya kuwarejeshwa kwao zaidi ya wakimbizi elfu 35 kabla ya muda uliopangwa walikabiliwa na changamoto mbalimbali wakati wa utekelezaji wa kazi yenyewe.



Moja ya changamoto ilikuwa ni baadhi ya wakimbizi kukataa kupanda mabasi  kwa kuhofia usalama wao huko waendako, hali iliyolazimu mbinu za ziada kuwashawishi kutumia.



Ili kuepuka machafuko, mkuu wa wilaya ya Kasulu Dany Makanga, viongozi na watumishi wengine wametoa raia kwa Watanzania kudumisha amani, utulivu na upendo miongoni mwao.



Wakizungumza  eneo la Musenyi nchini Burundi Lewisi Kisanja na John Claudio waliokuwa wakisubiri kwenda maeneo ya mikoa yao ya kuishi  wameiomba serikali yao ya  Burundi kuwalinda, kuwaendeleza kielimu na kuwapatia maeneo ya Kilimo.



Dotto Elias. TBC Kigoma.




Last Updated ( Thursday, 13 December 2012 11:33 )


 

TANZANIE - accès rapides

Actualités par pays

 

Newsletter


 
 
 
 
 
 

Actualités par pays

Newsletter


 
 
 
 
 
Tanzanie - Actualites